KIMENUKAA Diva na Godzilla Wapeana za uso huko Twitter - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

KIMENUKAA Diva na Godzilla Wapeana za uso huko Twitter

\
Rapper Godzilla na mtangazaji wa Clouds FM, Diva Jumanne hii wamebadilishana maneno makali kwenye mtandao wa Twitter.

Yote yalianza baada ya Zilla kudai kuwa sababu ya King Crazy GK kutofanya vizuri kimuziki ni kuwa na uhusiano na Diva.

“Acha nimsitiri saa Hii nimefunga ila ningekuwa sijafunga Pangechimbika afu zillah una shemeji mpya asa hivi anaitwa @HeriMuziki Gk is my ex,” alijibu Diva. “Hajafunga kim kardashian liar bring back GK yoo,” aliongeza Zilla.

“Stress zako za kufanya vibaya kimuziki usiniletee mimi fight your levels, hizo battle wapelekee wanaume wenzio wanaofanya hip hop kama ww,”aliendelea Diva. “@FezaKessy tell this madam the level of quality of my baby mama…she think am stressed…jokes on her @Divathebawse,” alijibu mapigo Zilla.

Diva alijibu, “Dude !go brush yo teeth achana na mimi, Go fight your levels ,thats gay kwanza kunirukia na maneno from nowhere, fanya mziki mzur acha kiki.”

“@Divathebawse shut the fuck up …dont mess with kings,” aling’aka King Zizi kabla ya Diva kumrukia na kumgusa paumapo zaidi, “King? Joke of the day, puliz billnass mtoto mdogo anakutoa mapovu embu chukua time uko usipick fight na mimi sio level yako. Tuheshimiane.”

“@Divathebawse unasema muziki mzuri kaa humuhttps://youtu.be/GCiPF80s_bE dont let clouds ruin you …you better than that,” aliendelea Godzilla.

Naye Diva aliendelea, “15 minutes of fame za kukujibu zimeisha … Usinijaribu Mimi sijaribiwi stak ugomvi na sitak mazoea ya Kijinga. Jiheshimu. Mambo ya mimi kuzaa yanakuhusu nini? kama kuzaa raha na wewe kazae, kapandikize mimba uzae achana na mimi wewe vipi wewe.”

Godzilla hakujibu tena!

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.