Juma Nature akananusha kulipwa na Harmorapa kwenye ‘Kiboko ya Mabishoo’ - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Juma Nature akananusha kulipwa na Harmorapa kwenye ‘Kiboko ya Mabishoo’

Msanii mkongwe wa muziki nchini, Juma Nature amevunja ukimya baada ya Harmorapa kumtuhumu kumdai pesa ya mavazi kwa ajili ya video ya wimbo wake mpya ‘Kiboko Ya Mabishoo’.

Akiongea na kipindi cha E News cha EATV Jumatatu hii, muimbaji huyo amesema rapper huyo chipukizi hana pesa ya kumlipa.
“Nikisema nimemlipisha Harmorapa pesa kwa ajili ya kolabo nitakuwa nakosea. Mimi ni mtu mzima nilikubali kufanya wimbo na msanii yule kwa sababu ni mkali na anajua muziki pia na imani atafika mbali. Hawezi kunilipa mimi, ana hela gani?,” amesema Nature.
Wiki chache zilizopita, Harmo alimlalamika msanii huyo mkongwe kupitia kipindi hicho kwa kusema, “Haipo sawa kwa wasanii wakubwa kutudai sisi ‘underground’ pesa ya kufanyia collabo wakati wanajua bado hata hatuanza kufaidika na muziki wenyewe.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.