HUYU NDO MTOTO WA BEN POL MWENYE VIPAJI VIWILI - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

HUYU NDO MTOTO WA BEN POL MWENYE VIPAJI VIWILI

Mtoto wa kiume wa Ben Pol, Mali ametimiza mwaka mmoja mwezi huu na tayari ameanza kuonesha makucha yake.
Ben ameiambia Bongo5 kuwa licha ya kuwa bado anawachanganya yeye na mama yake nini kinaweza kuwa kipaji chake, kuimba na kikapu ni vitu vinavyoelekea kuja kuwa passion ya mtoto wao.
“Ukimpa mpira anapenda kucheza sana kwa mikono, anapenda kudundadunda sana mpira,” amesema Ben Pol.
“Lakini vile vile pia mama yake anaimbaga naye mara nyingi sana, nyimbo za kitoto. Mama yake akiwa anaimba anamfuatisha sijui sauti ya pili, sijui anaimba sauti ya ngapi. Kwahiyo anaonekana anapenda kuimba, anapenda mpira, kwahiyo sijui itakuwaje, sijui atakuwa mcheza mpira sijui atakuwa muimbaji, lakini all in all nashukuru Mungu anakua vizuri,” ameongeza.
“Ila kiukweli kwenye kipaji hapo bado tunaendelea kuangalia sababu kiukweli anatuchanganya, atakuwa Shaquille O’Neal au atakuwa R.Kelly, hapo ndio au atakuwa Ben Pol au atakuwa Hasheem Thabeet.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.