Hizi ndiyo mechi atakazozikosa Pogba - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hizi ndiyo mechi atakazozikosa Pogba

Mchezaji ghali duniani Paul Pogba wa Manchester United anatarajiwa kukosa mechi mbili baada ya kuumia katika mchezo wa Europa League jana (Alhamisi) walipocheza dhidi ya FC Rostov ya Urusi.
Pogba aliumia katika dakika ya 48 ya kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na Marouane Fellaini. Katika mchezo huo ambao Man United walikuwa nyumbani katika uwanja wa Old Traford walishinda bao 1-0 lililofungwa na Juan Mata.
Mchezaji huyo anatarajiwa kukosa mchezo wa ligi kuu ya Uingereza wa Jumapili hii ambapo United itakuwa ugenini ikicheza dhidi ya Middlesbrough pamoja na mechi nyingine ya timu ya taifa ya Ufaransa wiki ijayo.
Akiongea na waandishi baada ya mchezo wa jana usiku, Mourinho alithibitisha hilo kwa kusema, “Kweli. Lakini sina uhakika, lakini kwa kweli hawezi kucheza dhidi ya Middlesbrough na hatachezea timu ya taifa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.