Harmorapa Huyu..Eti Amesema Hii Ndiyo Sababu ya Kumpigia Magoti Ali Kiba....!!!! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Harmorapa Huyu..Eti Amesema Hii Ndiyo Sababu ya Kumpigia Magoti Ali Kiba....!!!!

Msanii wa muziki wa hip hop, Harmorapa amefunguka kwa kudai kuwa Tanzania hajaona msanii wa kumfananisha na Alikiba na kusema hata ngoma yake ambayo amefanya na Juma Nature alitaka kufanya na Alikiba.

Rapper huyo alikuwa mmoja kati ya watu waliojitokeza JK Nyerere Airport kumpokea muimbaji huyo wa wimbo Aje kitokea Afrika Kusini.

Katika tukio hilo rapper huyo alionekana akipigia magoti muimbaji huyo huku akimkabidhi tisheti tukio ambalo lilizua maswali mengi.

Akiongea katika kipindi cha Enewz cha EATV, Harmorapa alidai yeye anamkubali sana Alikiba ndio maana akafanya kitendo hicho.

“Kiukweli King Kiba kwa Tanzania hapa sioni wa kumfananisha naye, kwa hiyo nisema sijaona bado wa kumlinganisha naye sababu jamaa anafanya vizuri sana na anajua muziki sana, hata kabla ya kurekodi hii kazi yangu mpya nilifanya jitihada na watu wa karibu na Alikiba japo niweze kufanya naye kazi lakini sikuweza kufanikiwa kutokana na mambo yake kuwa mengi sana na watu pia ambao walikuwa wakinipa connection naye kuna vitu sikuweka sawa, na muda nikaona unazidi kwenda nikasema ngoja nifanye tu” alisema Harmorapa

Aliongeza, “Hata ishu ya kumpigia magoti ni kuonyesha kwamba namkubali, ni heshima kwake, sidhani kama kuna tatizo hapo,”

Rapper huyo hivi karibuni ameachia wimbo wake mpya ‘Kiboko ya Mabishoo’ akiwa amemshirikisha Juma Nature.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.