Hamorapa Amuomba Radhi Diamond - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hamorapa Amuomba Radhi Diamond

\
Harmorapa amemuomba radhi Diamond baada ya akaunti yake ya Instagram kutumika kumtukana hitmaker huyo wa Marry You.

Rapper huyo amepost kipande cha video kwenye mtandao huo akisema kitendo hicho hakufanya yeye bali kuna watu walihack akaunti yake hiyo.

“Followers wangu, mashabiki wangu nasikitika kitu kimoja toka asubuhi leo (jana) nashindwa kuingia katika akaunti yangu,” amesema Harmo kwenye video hiyo.

“Kuna watu wamehack akaunti yangu na kupost vitu ambavyo sio vizuri ni vyaajabu sana. Mimi binafsi siwezi kumtukana Diamond wala kumtukana Alikiba pia na P Funk Majani ambaye nipo naye kwenye mizunguko yangu leo kwa Mx Carter kwa kunisaidia kuirudisha akaunti yangu,” ameongeza.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.