Habari Njema: WhatsApp Warudisha 'Status' Ila Sasa Kuitwa 'About' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Habari Njema: WhatsApp Warudisha 'Status' Ila Sasa Kuitwa 'About'

Mtandao wa Mawasiliano kwa njia ya internet wa WhatsApp wenye watumiaji zaidi ya bilioni moja duniani kote umerudisha mfumo wake wa zamani wa kuandika 'status' kwa njia ya maneno.

Mfumo huo ambao uliondolewa siku za karibuni na kuletwa wa kuweka 'status' kwa picha na video fupi ulionekana kuhitajika zaidi na watumiaji wengi kutokana na urahisi wake kwa watumiaji.

Kupitia mitandao mbalimbali watumiaji wengi wa walitoa malalamiko kwa menejimenti ya WhatsApp na kutaka mfumo wa zamani urudishwe ili iwe rahisi kwao kuweka 'status' kwenye namba zao.

Kurudishwa kwa mfumo huu ni uthibitisho kuwa malalamimo yao yamesikilizwa na yalikua na mashiko.

Ili kuweza kupata mfumo huu wa kuandika 'status' kwa njia ya maneno kama zamani unapaswa u 'update' WhatsApp yako kwa kuingia play store.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.