Flora Mbasha Adaiwa Kupigwa Mimba - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Flora Mbasha Adaiwa Kupigwa Mimba

WAKATI vikao vya harusi yake vikiwa vinaendelea kusubiri kufunga ndoa Aprili mwaka huu, nyota mkubwa wa nyimbo za Injili, Madame Flora, ambaye ni maarufu zaidi kama Flora Mbasha, anadaiwa kupata ujauzito, Risasi Mchanganyiko limetonywa.


Flora Mbasha
Chanzo makini kilicho karibu na mwimbaji huyo ambaye ndoa yake ya kwanza na mumewe Emmanuel Mbasha ilivunjwa na mahakama hivi karibuni, kilisema tayari ana ujauzito unaokadiriwa kuwa na umri kati ya miezi miwili au mitatu, ambao umeanza ‘kumsumbua’ kiasi cha kushindwa kufanya shughuli zake vyema.

“Hivi mnajua kama Flora (Mbasha) ni mjamzito? Basi kwa taarifa nilizonazo ni kuwa wakati vikao vya ndoa yake inayotarajiwa kufungwa mwezi ujao vikiendelea, imebainika kuwa ni mjamzito, jambo ambalo limezua minong’ono kwa baadhi ya waimbaji wenzake wakihoji imekuwaje mtumishi huyo wa Mungu kubeba mimba kabla ya ndoa?” kilisema chanzo hicho.


Flora Mbasha
Kuhusu ndoa yake hiyo, chanzo hicho kilisema hakuna mabadiliko juu ya shughuli hiyo, isipokuwa gumzo kubwa miongoni mwa waimba Injili ni suala hilo la ujauzito. Risasi Mchanganyiko lilimtafuta mwimbaji huyo ambaye alipopatikana na kuulizwa juu ya suala hilo, hakukataa wala kukubali, isipokuwa alisema kama ni kweli jambo hilo lipo, basi ni kitu cha kheri.
“Mimi sijui unachokizungumzia kinaanzia wapi, lakini kama ni kweli hivyo unavyosema, basi ni jambo la kheri kwa sababu siku zote watoto ni Baraka,” alisema kwa kifupi na kumwambia mwandishi ni vyema kama wataongelea kuhusu albamu yake ijayo.

“Nipo katika maandalizi ya mwisho ya albamu yangu mpya, nategemea kuizindua wakati wa Pasaka mwaka huu, hii itakuwa ni albamu yangu ya sita ambayo itakuwa tayari wakati wowote kuanzia sasa,” alisema.

Baada ya kuachana na Emmanuel Mbasha, Madame Flora alikuwa akitoka kimapenzi na kijana anayejulikana kwa jina moja la Peter anayedai kuzaa mtoto na mwimbaji huyo. Hata hivyo, uhusiano huo ulivunjika siku chache zilizopita ndipo zilipopatikana habari za kutaka kuolewa na mwanaume mwingine anayetajwa kwa jina la Daudi inayotarajiwa kufungwa Aprili 30, mwaka huu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.