Everton ya Uingereza kutua nchini hivi karibuni - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Everton ya Uingereza kutua nchini hivi karibuni

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga amekutana na muwakilishi wa Sports Pesa Tanzania, Luca Neghesti kumpa taarifa Waziri huyo kuhusu maandalizi ya kuileta timu ya Everton inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza kwa ajili ya kucheza mechi za kirafiki hapa nchini.

Waziri huyo pia amekutana na wawakilishi wa timu hiyo jana ofisi kwake jijini Dar es salaam kwaajili ya ziara hiyo hapa nchini.
Aidha Waziri Mahiga alisema ziara hiyo itasaidia kuitangaza Tanzania duniani pamoja na kuhamasisha mchezo wa mpira wa miguu kwa vijana wa Kitanzania.
Hizi ni baadhi ya picha walizopiga kwa za pamoja:Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.