England yachapwa na Ujerumani - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

England yachapwa na Ujerumani

Lukas Podolski akishangilia goli alilofunga

Timu ya taifa ya England imekubali kichapo cha bao 1-0 ugenini dhidi ya timu ya taifa ya Ujerumani katika mchezo wa kirafiki.

Bao pekee la ushindi katika mchezo huo liliwekwa kambani na mshambuliaji Lukas Podolski katika dakika ya 69 ya mchezo kwa shuti kali la umbali wa mita 25 lilomshinda kipa wa England Joe Hart.

Mchezo huu wa kirafiki ulikua ni mchezo wa mwisho kwa mshambuliaji huyu wa timu ya taifa ya Ujerumani Lukas Podolski anayestaafu soka la kimataifa akiwa na umri wamiaka 31.
Podolski akirushwa juu na wenzake baada ya mchezo kumalizika ikiwa ni sehemu ya kuuga nyota huyo mwenye miaka 31

Mshambulia huyu alianza kuichezea timu ya taifa ya wakubwa mwaka 2004 na kufunga jumla ya magoli 49 katika michezo 130.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.