Chris Brown Aripotiwa Kukabiliana na Addiction ya Dawa za Kulevya. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Chris Brown Aripotiwa Kukabiliana na Addiction ya Dawa za Kulevya.

Mambo yanazidi kumwendea kombo Chris Brown. Kwa mujibu wa watu wake wa karibu, muimbaji huyo ameshindwa kabisa kuacha kutumia dawa za kulevya ambazo zimesababisha kuharibu maisha yake binafsi na ya kikazi.

Mtandao wa Billboard umeanda makala iliyopewa jina ‘Chris Brown’s Downward Spiral’ inayoangaza maisha yake ya miaka mitatu iliyopita binafsi na kimuziki. Watu wake wa karibu wanajadiliana kuhusu matumizi ya dawa za kulevya ambazo wanazielezea kama kucheza na kifo.

“He will cuss you out and say, ‘Hey, man, I’m functioning. I’m going to get the work out.’ And he does,” mmoja wa watu wa karibu anasema. “But [he’s not] the first functional star who thinks they can handle those powerful drugs. I got to say with all my heart, he’s dancing with death.”

Watu hao wanasema dawa anazotumia ni pamoja na Xanax, lean, na cocaine. Mmoja wa walinzi wake wa zamani amesema madawa hayo yameathiri kwa kiasi kikubwa mood yake.

Mtu mwingine aliyewahi kufanya kazi naye anasema, “Sober Chris is a solid guy with a big heart. High Chris and Chris coming off drugs is ungrateful, unappreciative and a foul person who most people don’t want to deal with. Good Chris? You’ll fight for him. Unfortunately, the last couple of years, it has been drug Chris. That Chris is not a good dude.”

Kutokana na matatizo hayo, watu wengi wamemkimbia Chris. Kwa mujibu wa makala hiyo ya Billboard kwa sasa Brown hana mwakilishi wake binafsi, timu ya ulinzi wala meneja.

Pia maisha yake binafsi yameharibika ikiwemo kuachana na Karrueche Tran.

“He’s always on social media, looking up who Karrueche was with, what she was looking like, what club she was at, who posted to her Instagram,” kimesema chanzo kimoja. Hivi karibuni Tran aliomba kuzuiliwa kwa Chris asimsogelee kwakuwa aliwahi kumpiga na kwamba hivi karibuni alimtishia kumuua.

Pamoja na watu wengi kumkimbia, wapo watu wanaoendelea kuwa naye akiwemo Brandy, ambaye amemsifia akisema, “Chris is an incredible singer and stylist who knows exactly who he is as an artist. As a whole, he’s courageous. I loved working with him [on 2012’s ‘Put It Down’] and would like to work with him again.”

Label yake pia, RCA, ipo nyuma yake. “We’re proud to be in business with Chris, a uniquely gifted artist who is always striving to be better,” they said. “Through his ups and downs, we will continue to stand behind him.”

Choreographer wake wa muda mrefu, Flii Stylez anadai kuwa Brown ameshindwa tena kuamini watu na hivyo kumfanya ajitenge na watu wengi akiwemo yeye mwenyewe. “He lost Rihanna and Karrueche, two people he loved. Right now, he doesn’t trust anybody. I’m probably the one who loves him the most out of everybody who is not his real family, and he won’t even talk to me. I can’t get to him. My brother is going through a lot. But he’s not crazy. This isn’t why I invested all this time into him. He goes in and out of being angry, but we want to see Chris dancing and singing.”

Mwaka huu Brown ataachia album mpya iitwayo, Hearttbreak on a Full Moon.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.