Barnaba Asema Bora waibiwe na Diamond kuliko kuibiwa na mtu binafsi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Barnaba Asema Bora waibiwe na Diamond kuliko kuibiwa na mtu binafsi

Barnaba amedai kuwa ni bora fedha zao za muziki ziibiwe na Diamond kupitia tovuti yake ya kuuza muziki ya Wasafi.com kuliko watu wengine.
Muimbaji huyo ameiambia Dizzim Online, “Tumeibiwa sana wasanii, tumedhulumiwa sana. Mungu anisamehe kidogo, bora atuibie msanii mwenzetu, tunajua msanii mwenzetu anakula yupo kwenye soko letu kuliko atuibie mtu binafsi.”
“Na yeye akiwa kama CEO [Diamond] alichukua uamuzi wa busara kama heshima kutupigia simu wasanii wenzake mwenyewe kuliko kuwatuma menejimenti. Mimi naona jambo zuri la bahati alilolifanya na nilienda nikachukuwa contract yangu na kiukweli nimeusaini lakini bado kuurudisha,” ameongeza.
Katika hatua nyingine hitmaker huyo wa ‘Lover Boy’ amewataja wasanii ambao watasikika kwenye albamu yake mpya. Wasanii hao ni pamoja na Baraka The Prince, Linex, Dela, H_art The Band, Bahati wa Kenya, Vanessa Mdee kuna Jux, Maua Sama, G Nako na wengine.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.