Barcelona Yaandika Historia kwa Ushindi wa 6-1 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Barcelona Yaandika Historia kwa Ushindi wa 6-1

Neymar alin'gara katika mchezo huu

Barcelona wamebirua matokeo ya kutinga nusu fainali kwa kuizaba Paris Saint Germain kwa mabao 6-1 katika mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Ulaya.

Sergi Roberto alifunga bao la 6 kwa mkwaju wa mwisho wa mchezo, na hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa 6-5 kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Nou Camp.

Barcelona walifunga magoli matatu katika dakika saba za mwisho. Walikuwa wakiongoza kwa 3-1.

Wiki tatu zilizopita PSG iliifunga Barcelona magoli 4-0 mjini Paris.

Hatua ya kurejesha magoli yote hayo ni kubwa kuwahi kushuhudiwa katika historia ya UEFA, na sasa Barcelona wana kila nafasi ya kunyanyua kombe la Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu.

Katika mchezo mwingine, Pierre Emerick Aubameyang alipachika 'hat trick' na kuipeleka Borussia Dortmund katika robo fainali dhidi ya Benfica
Aubameyang alifunga magoli matatu

Borussia Dortmund wameshinda kwa jumla ya magoli 4-1 katika mechi mbili walizocheza.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.