Azam imeshindwa kufuzu hatua ya makundi michuano ya CAF - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Azam imeshindwa kufuzu hatua ya makundi michuano ya CAF

Azam FC wametupwa nje ya mashindano ya Caf Confederation Cup kufatia kipigo cha magoli 3-0 ugenini dhidi ya Mbabane Swallows ya Swazland.

Mchezo wa kwanza ulichezwa Jumapili iliyopita kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi-Dar es Salaam, Azam walipata ushindi mwembamba wa goli 1-0.

Kichapo cha goli 3-0 kilichoiondoa Azam mashindanoni, kimekuja siku moja baada ya mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Yanga SC kuondoshwa kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika na Zanaco FC ya Zambia. Yanga wameangukia kwenye michuano ya Caf Confederation Cup.

Kumekuwa na videos na picha zinazosambaa zionesha viongozi wa Azam wakilalamika kufanyiwa fujo na mashabiki wa Mbabane kabla ya mchezo pamoja la malalamiko ya kupulizwa kwa dawa zinazoaminika kuwa na kemikali kwenye vyumba vya kubadilishia nguo walivyopewa Azam FC.

Mbabane wanasonga mbele kwa ushini wa jumla ya magoli 3-1 baada ya michezo miwili dhidi ya Azam FC.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.