Arsene Wenger Amlaumu Refa Kwa Kipigo Cha 5 - 1 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Arsene Wenger Amlaumu Refa Kwa Kipigo Cha 5 - 1

Mashabiki wa Arsenal wabeba bango la kumtaka Arsene Wenger kuondoka.

Arsene Wenger anasema kuwa alikasirishwa na refa baada ya kikosi chake cha Arsenal kilichoonyesha ushujaa kubanduliwa katika mashindano ya kombe la vilabu bingwa Ulaya na Bayern Munich.

Refa Anastasios Sidiripoulos aliwanyima Arsenal mkwaju wa penalti wakati walipokuwa 1-0 kabla ya kuwpatia Bayern penalti baada ya Laurent Koscielny kumfanyia Robert Lewandowski madhambi katika lango.

Koscielny baadaye alitolewa nje huku Arsenal ikipoteza 5-1 siku ya Jumanne na 10-2 kwa jumla.

''Penalti na kadi nyekundu haziwezi kuelezewa zilikotoka na ni kama kashfa'', alisema Wenger.

Refa alishindwa kutekeleza jukumu lake vilivyo.Inaniwacha nikiwa na hasira na kunivunja tamaa.

Arsenal ilianza mechi hiyo ikijua kwamba ingehitaji magoli mengi kuweza kuibandua Bayern baada ya wageni hao kuwashinda kwa magoli 5-1 nchini Ujerumani wiki tatu zilizopita.

Shambuilio la Theo Walcot katika kipindi cha kwanza liliwapatia matumaini Arsenal ,lakini matumaini hayo yakafifia wakati Lewandowski alipofunga kupitia penalti huku Koscielny akpewa kadi nyekundu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.