Arsenal ni sikio la kufa,yapigwa 3-1 na West Bromwich - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Arsenal ni sikio la kufa,yapigwa 3-1 na West Bromwich

Craig Dawson akiwa hewani juu ya Nahodha wa Arsenal, Laurent Koscielny kuifungia West Bromwich Albion bao la kwanza dakika ya 12 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya timu ya kocha Mfaransa, Arsene Wenger katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa The Hawthorns. Dawson alifunga mabao mawili na la tatu dakika ya 75, huku la pili la West Bromwich likifungwa na Hal Robson-Kanu dakika ya 55 na la kufutia machozi la Washika Bunduki wa London, likifungwa na Alexis Sanchez dakika ya 15

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.