Vitu 4 Vilivyoielezea Kuwa Diamond Ni Mtu Wa Hulka Gani Kwenye Interview ya Leo Tena ya Clouds. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Vitu 4 Vilivyoielezea Kuwa Diamond Ni Mtu Wa Hulka Gani Kwenye Interview ya Leo Tena ya Clouds.

Kupitia interview ya Diamond na mchumba wake Zari kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, nimeweza kubaini mambo haya manne kuhusiana na hulka ya Diamond.

1. MNYENYEKEVU.

Wakati Diamond alipoingia kwenye kituo cha Clouds pamoja na mke wake Mama Tiffa maarufu kama Zari the Boss Lady, watangazaji wa Clouds FM akiwemo Hussein na wenzake walimwekea muziki wa asili pale kwa maana acheze. Diamond kwa mihemko na mbwembwe alisimama na la ziada ukitazama kwenye video aliyoirusha kupitia account yake ya Youtube, inaonyesha akimuinua Zari kutoka kwa kiti chake ilikujiunga naye kucheza mdundiko. Hii inatoa muktadha kuwa, Diamond licha ya mafanikio anayoyapata katika muziki lakini pia hutii bila kujali anavyoambiwa na mtu yeyote afanye jambo fulani.

Maana sio wote mastaa wakubwa watakaopewa muziki wa asili waambiwe wacheze wakacheza, wengi wangeona watangazaji hawa wanazingua tu ama kuwakejeli kwa maana kwa hao ni mastaa na kwa mfano vile Diamond anavyopeta hadi bara Ulaya na Marekani.

2. HESHIMA KWA MPENZI WAKE


Katika interview hiyo, Zari alifunguka na kusema kuwa kitu anachompendea mchumba wake Diamond, huwa hapendi kugusa simu yake na yeye pia vivyo hivyo. Maneno haya kutoka kwa Mama Tiffa, yanatoa tafsiri kuwa Diamond anaheshimu vitu vya mkewe na thawabu yake imeongeza ladha kwenye mapenzi yao ambayo ukweli wake uko wazi kwa kila mtu na wengi wanatamani wawe kama hao katika mahaba.

3. ANA MAPENZI YA DHATI KWA WATOTO WAKE

Majibu ya Zari alipokuwa ameulizwa swali na kama wawili hao hukosana katika shughuli zao za kila siku wanapokuwa nyumbani, yalibaani wazi jinsi Diamond anavyowapenda watoto wake hasa Tiffa ambaye Zari alisema kuwa huwa chanzo cha ugomvi baina ya Baba Tiffa na Mama Tiffa pale Zari anapochukua hatua ya kumuadhibu Tiffa anapokosea. Zari anasema Diamond kwa mara nyingi, huwa anateta na hataki kuona mtoto wao huyo ananilia kisa na maana kaadhibiwa.

4. ANA BUSARA NA MVUMILIVU KATIKA MAHUSIONO YAO

Suala la mahusiano kati ya watu wawili wapendanao huwa sio jambo rahisi, hasa ilikizingatia kuwa watu ambao wako kwenye mahusiano hayo wawe ni maarufu kama ilivyo kwa Diamond na mpenzi wake Zari. Akigusia suala hili, Zari alisema yeye hutongozwa kila siku na watu mbalimbali. Kama tujuavyo na nikinukuu maneno ya Zari ” On my phone mimi ni businessperson yeye ni businessperson, kunatokea vitu vingine message zingine kwahivyo huwezi kujua ninini itatoka.

Watu wananitongoza kila siku na anajua and he is a superstar, he is young and succeful obvious kuna watu wanamfuata. In our relationship one has to be strong, if you don’t put other things aside you will die.” Sentensi hii imebeba uzito wa hulka ya uvumilivu katika mahusiano ya msanii Diamond kwani wivu ni kitu cha kawaida kwa binadamu wa kawaida na Diamond si malaika hivyo ni lazima husikia wivu kwa mke wake anapotongozwa, hivyo kwa busara aliyonayo inamuepusha na zimwi la kuvunjika kwa ndoa ya sababu ya wivu na kukosa uvumilivu katika mahusiano.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.