Unafahamu Irene Uwoya Anatamani Kufanya Nini Mbali na Kuigiza ? - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Unafahamu Irene Uwoya Anatamani Kufanya Nini Mbali na Kuigiza ?

Kila mtu maishani mwake ana kitu ambacho anatamani sana kukifanya ingawaje kukifikia ni lazima uhangaike sana pengine hii ni kutokana na mazingira yetu hili lipo pia kwa Muigizaji maarufu nchini Irene Uwoya ambaye hajawahi kufikiria kuwa muigizaji na kazi hiyo havutiwi nayo kabisa bali anatamani kuwa Mchungaji (Pastor).

Irene Uwoya amesema tangia akiwa mdogo alikuwa anapenda sana kusali mchana na usiku na alifikiria kuwa siku moja angekuja kuwa mchungaji mkubwa sana ingawaje ndoto hizo zikaja kupotea baada ya kukutana na marehemu Kanumba kwani alijikuta akiingia kwenye Tasnia ya Bongo Movie na kupoteza wito wake wa uchungaji.

“Kusema ukweli mbali na uigizaji natamani sana kuwa Pastor kwani nakumbuka nilivyokuwa mdogo nilikuwa nasali sana yaani nilikuwa na ndoto ya kuwa mchungaji mkubwa sana lakini baada ya kuanza kukutana na akina Kanumba nikaanza kupenda kuigiza“Alisema Irene Uwoya kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.