Siwema: Nay Alinitapeli Milioni 7 Hivi Hivi Najiona, Sitasahau ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Siwema: Nay Alinitapeli Milioni 7 Hivi Hivi Najiona, Sitasahau !

MZAZI mwenzake na staa wa Hip Hop Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema ameibuka na kutoa simulizi yake ya nyuma na kusema kamwe hatasahau mzazi mwenzake huyo alivyomuongopea na kumpiga shilingi milioni 7 taslimu.

Siwema aliivujisha ishu hiyo hivi karibuni wakati mwanahabari wetu alipomtaka aseme kitu gani ambacho hatakisahau kutoka kwa mpenzi wake huyo wa zamani ndipo mrembo huyo alipofunguka hayo lakini akasema hata hivyo, alishasamehe kwa sababu yalitokea kwenye kipindi ambacho penzi lilikuwa motomoto.

“Si unajua tena mtu ukikolea, kuna kipindi aliniambia ametaitiwa polisi, zinahitajika hela, nilipata mshtuko kweli, ikabidi niende benki haraka, nikamtumia. Nilishasamehe maana tuliyazungumza na tukiwa kama wapenzi yaliisha, ila sitasahau aisee,” alisema Siwema.

Alipotafutwa Nay ili kumsikia kama ana lolote kuhusu ishu hiyo, simu yake iliita kwa nyakati tofauti bila kupokelewa kwa takriban wiki tatu mfululizo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.