Shamsa Ford Asema Ana Mpango wa Kufungua Chuo cha ‘Kudansi’ - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shamsa Ford Asema Ana Mpango wa Kufungua Chuo cha ‘Kudansi’

Hii ni tofauti kidogo na namna ambavyo tumewazoea mastaa wetu kadhaa ambao wengi kwenye mahojiano yao huweka wazi mipango ya baadae ambayo mara nyingi huzunguka na aina ya kazi anayofanya kama ni msanii wa muziki utasikia akisema anataka kuwa na studio yake au kama mtu wa filamu atasema anataka kuwa na kampuni ya kutengeneza filamu.

Hii ni tofauti kwa Actress kutoka Bongo Movie Shamsa Ford ambaye yeye amesema mipango yake ya baadae ni kuwa na chuo kitakachokuwa kinajishughulisha zaidi na kufundisha watu kucheza (choreographers) na amesema kuwa kudansi imekua ni kazi ambayo alikua anaota kuifanya toka akiwa mdogo na sio filamu.

Shamsa Ford ameongeza kwa kusema alishamtafuta Msami wa THT kuzungumza nae kuhusu nia yake hiyo na anachokitafuta kwa sasa ni kupungua kwa mwili wake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.