Rich Mavoko Adai ‘Kokoro’ Alikuwa Amshirikishe Msanii wa Nigeria Lakini Alileta Chenga - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Rich Mavoko Adai ‘Kokoro’ Alikuwa Amshirikishe Msanii wa Nigeria Lakini Alileta Chenga

Rich Mavoko amedai kuwa kwenye wimbo wake Kokoro, ni msanii wa Nigeria ndiye alikuwa amepangwa kushirikishwa.

Hata hivyo amedai kuwa baada ya msanii huyo kuwa na kona nyingi, alimuomba bosi wake, Diamond akae mwenyewe.

“Kuna msanii alitakiwa akae kutoka Nigeria mishe zikawa nyingi hapa na pale, hivi imekuwa hivi, vile imekuwa hivi, tutafanya hivi, muda unaenda. Nilikuwa na wimbo mmoja Ibaki Story kwahiyo watu walikuwa wanataka wimbo mwingine kabla ya mwaka kuisha. Nikamwambia D ‘kama imeshindikana kwanini usifanye wewe, kaa humu wewe.’ Akaniambia hakuna tatizo, mimi nilijua wewe mwenyewe unamfikiria sana huyu jamaa.’

Pengine huo ulikuwa ni uamuzi muhimu zaidi kwakuwa Kokoro umekuwa wimbo wenye mafanikio kiasi cha kupewa tuzo ya wimbo wa mwezi na kipindi cha XXL cha Clouds FM.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.