Ray C Mpya Kurudhiswa Kwa Kishindo na Valentine's Day - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ray C Mpya Kurudhiswa Kwa Kishindo na Valentine's Day

‘MAPENZI matamu,
Niwapo nawe mpenzi,
Sioni mwingine wa kufanana na wewe,
Nitalienzi penzi lako sitokuacha hasilani.
Ni sanaa ya hali ya juu kabisa kutengeneza wimbo ambao unakwenda mtaani kuimarisha uhusiano uliolegea, kurudisha penzi lililotaka kupotea, kuwapa utulivu walioumizwa na mapenzi, kuifunza jamii kuwa mbali na ulaghai mwingi uliopo bado kuna mapenzi ya kweli hakika kwa tungo zile Rehema Chalamila ‘Ray C’, alituweza.
Hivi ni nani kati yetu ambaye hakuwahi kuvutiwa na moja kati ya nyimbo nyingi za Ray C? Ni ngumu kukwepa hili maana kipindi hicho nyimbo za mkongwe huyu aliyepachikwa jina la ‘Kiuno Bila Mfupa’ zilitumika kama ‘dedication’ katika uhusiano mwingi wa mapenzi.
Kumbuka kuwa kimya kingi kina mshindo mkubwa, tukiwa tunaisubiri kwa hamu siku ya wapendanao hapo Februari 14 tayari masikioni mwetu tumeanza kusikia ile sauti tamu tuliyoikosa kwa muda mrefu kutoka kwa Ray C.

Ijumaa ya wiki iliyopita alikuwa mkoani Dodoma na kupata fursa ya kutumbuiza wimbo wake unaoitwa Umenikataa mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Siyo Ray C yule aliyetuhuzunisha mwaka jana huyu ni mpya kabisa mwenye kasi na kiwango cha kuwa msanii bora endapo akiendelea kukaza. Tayari amefanya kava ya wimbo wa mdogo wake Recho unaoitwa ‘Upepo’ ambao unaopatikana mtandaoni.

Hali kadharika ameonekana akipiga tizi pale nyumba ya vipaji (THT) na kushiriki kuandaa (Valentine Collection Album) inayoandaliwa na Ema The Boy wa Epic Record itakayotoka hivi karibuni.

Haitoshi anakwenda kuwapa burudani mashabiki wake siku ya wapendanao, Februari 14 akiwa na Barnaba, anaweka muda wake mwingi kwenye kazi ambayo kipindi hiki ameipa kipaumbele zaidi kuliko chochote kile.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.