Ray C Akunwa na Uandishi wa Rayvanny 'Nampenda Sana Yule Mtoto Anaandika Sana Mashairi' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ray C Akunwa na Uandishi wa Rayvanny 'Nampenda Sana Yule Mtoto Anaandika Sana Mashairi'

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva Ray C ni moja ya wasanii wanaomkubali sana Rayvanny kutoka WCB na sio tu kwa staili yake ya uimbaji bali pia anavutiwa sana na uandishi wake wa Mashairi.

Ray C amesema Rayvanny bado ni mdogo kiumri lakini kwa alipofikia na uwezo wake wa utungaji wa mashairi bila shaka yoyote atafika mbali sana kwenye muziki kwani hata yeye kwa sasa anatamani kufanya nae kazi.

“Nampenda sana yule mtoto Rayvanny, anaandika sana mashairi, nasikia anaandikia wasanii wengi nyimbo, hata mimi natamani kufanya naye kazi na naamini atafika mbali sana kimuziki” alisema Ray C kwenye mahojiano yake na Kituo cha East Africa Radio.

Hata hivyo Ray C kwenye mahojiano hayo amewaahidi mashabiki wake kuwa amejipanga vilivyo kurudi kwenye Game kwani anajua nafasi yake kwenye muziki bado ipo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.