Ray C Aahidi Kurudi kwa Kishindo Kwenye Game. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ray C Aahidi Kurudi kwa Kishindo Kwenye Game.

Msanii wa Bongo Fleva Ray C ameahidi kurudi kwa kishindo kwenye Game baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kutokana na matatrizo ya kiafya yaliyokuwa yanamsumbua.

Ray C aliyasema hayo baada ya kutumbuiza kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri cha Mkoa wa Dodoma (RCC) Juzi,ambapo ameweka wazi kwamba yupo mbioni kurudi upya katika muziki wa ushindani kwa kuwa anaamini bado muziki wake una mashabiki wa kutosha.

“Narudi kwa kasi, kama ulivyoona watu bado wananikubali, hayo mengine Mungu anasaidia naendelea vizuri,’’Ray C aliliambia Gazeti la Mtanzania .

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.