Rapa Nikki Mbishi Kuja na Nyimbo za Kisingeli Baada ya 'I'm Sorry JK' Kufungiwa na BASATA. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Rapa Nikki Mbishi Kuja na Nyimbo za Kisingeli Baada ya 'I'm Sorry JK' Kufungiwa na BASATA.

Rapa Nikki Mbishi ameamua kuingia rasmi kwenye aina ya muziki wa Kisingeli baada ya wimbo wake wa ‘I’m sorry JK’ kufungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) .

Nikiki Mbishi kupitia ukurasa wake wa Instagram ameanza kwa kuwaomba radhi mashabiki wake kwa wimbo huo wa I’m Sorry JK kufungiwa kwa kuandika “Salaam,Baada ya salamu naomba niombe radhi kwa vyombo vyote vya habari kuwa sitoweza kuwapa ushirikiano wowote kuhusu wimbo wangu wa “I’M SORRY JK” uliositishwa na hii ni kwa usalama wao na wangu pia.Napokea simu nyingi sana zikihitaji maelezo juu ya suala hilo ila kiukweli kwa watakao hitaji taarifa kamili wanaweza kufika ofisi za BASATA,naomba nisiwe msemaji tena juu ya jambo hili.”

Baada ya kuwaomba radhi ndipo akawahakikishia mashabiki wake ujio wa kazi zake mpya kwa kuandika “#Asanteni sana,naomba msubiri ujio wangu mpya wa #SINGELI na aina nyingine za muziki kama #NAIJA #MCHIRIKU n.k. MUZIKI NI AJIRA,MUZIKI NI KAZI YANGU.“

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.