Professor Jay Awachana Wadau wa Hip Hop Wenye Wivu wa Kijinga. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Professor Jay Awachana Wadau wa Hip Hop Wenye Wivu wa Kijinga.

Msanii mkongwe wa Hip Hop nchini Professor Jay ameamua kuwatolea uvivu wadau na wasanii wa hip hop ambao wana wivu kwa baadhi ya wasanii wa Hip hop hauwezi kusaidia muziki wa Hip hop kufika mbali.
Haya yote yamejiri baada ya mwaka jana kufanya vizuri na ngoma yake ya Hip Hop Singeli ‘Kazi Kazi’  na kuwepo kwa baadhi ya wasanii ambao waliupokea vizuri na baadhi ya wasanii wa hip hop walionesha kutouelewa, huku wengine wakisema Prof Jay amepotea kwa kutoa ngoma ya aina hiyo.
Professor Jay amesema wakati anatunga na kuandaa ngoma hiyo ya Hip hop Singeli alitambua wazi kuwa wapo watu wataipenda na wapo watu wengine hawataipenda, lakini kwa asiyeipenda kazi hiyo asilazimishe kila mtu kutaka kuichukia kazi hiyo.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika “Kila mtu ana haki ya kupenda ambacho moyo wake unamwambia, tunakosea sana kutaka wote wapende kile tunachokipenda. Kupinga mtu aliyefanikiwa hakukupi uhalali wa wewe kufanikiwa, tuna nafasi ya kujirekebisha na kupeleka hip hop yetu mbali ila siyo kwa wivu” 
Mbunge huyo wa mikumi ameendelea kwa kujibu kile kilichosemwa na Nash MC kuhusu singeli kwenda kimataifa ambapo amesema kuwa watu wanaohoji hilo wanakosea sana kwani wao wanatakiwa kujiuliza kwanini muziki wa hip hop hauvuki ‘boda’ na kufika level hizo za kimataifa.
“Juzi tu dogo Nash MC aliuliza, eti kama tayari singeli imeshakwenda International? Nilitegemea angeuliza kwa nini hip hop  ya bongo haivuki boarder? Mkafurahia kishabiki bila kujiuliza hip hop ndiyo imezaa karibu aina zote za muziki wa kizazi kipya lakini mbona wasanii wake hawafiki mbali, matokeo yake baadhi ya wasanii wanaojiita wa Hip hop na mashabiki wao wanaichukia aina nyingine ya muziki kwa mafanikio wanayopata wenzao. Badala ya kujiuliza tumekosea wapi sasa tunakuwa na wivu wa kijinga na kuchukia mafanikio ya wengine waliopambana kufika hapo walipo sasa”Amesema Professor Jay
Prof. Jay alizidi kusisitiza kuwa mapinduzi ya hip hop yaliofanywa na wasanii wa zamani yaliongozwa kwa upendo ndani yake na si chuki “Mapinduzi yaliyofanywa na Kwanza Unit, Saleh Jabri, HBC, Sugu, Hashim, Majani, GWM, Solo, Afande, Jay Moe n.k yalifanikiwa kwa upendo siyo chuki, hata wanaojitahidi kupeperusha bendera ya  hip hop kama Fid Q, Joh Makini watu wanawakatisha tamaa, I RESPECT YOUR HUSTLE my young brothers. Matokeo yake hao wanaopinga wenzao wanaoonesha juhudi, wanaishia kuimbia washkaji zao kwenye vibanda vya kahawa, You need to grow up”. 
Amemaliza kwa kusema kizazi hiki cha kisasa cha hip hop ni kama cha makambale kila mtu ana ndevu Hajulikani Baba,Mama wala Mtoto “Kizazi hiki cha hip hop kimekuwa kama ukoo wa kambale, yaani baba, mama na watoto wote wana ndevu, kila mtu akiambiwa mkali anajiona kweli kamaliza, hii heshima mliyoikuta kwenye hip hop tuliitafuta kwa jasho na damu, kisha mnaichukulia poa tu, badala ya kwenda mbele mnarudi nyuma kwa kasi”. 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.