Picha: Defoe Akubali Kulala na Bradley Lowery Kwenye Siku Yake ya Mwisho Duniani. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Picha: Defoe Akubali Kulala na Bradley Lowery Kwenye Siku Yake ya Mwisho Duniani.

Jumamosi ya leo ndio siku ambayo ilidaiwa kuwa mtoto ambaye ni shabiki mkubwa wa klabu ya soka ya Sunderland, Bradley Lowery atafariki dunia kutokana na ripoti ya madaktari ambapo anasumbuliwa na maradhi ya kansa ambayo imedaiwa kufika mwisho hadi kushindikana kutibika.

Bradley amemuomba Jermain Defoe kulala naye kitanda kimoja hospitalini ambapo amelazwa katika siku yake hiyo ya mwisho duniani ambayo alidaiwa kuwa atafariki ambapo mshambuliaji huyo amelikubali ombi hilo.
Miezi kadhaa iliyopita ilidaiwa kuwa matibabu ya mtoto huyo yatagharimu kiasi kisichopungua bilioni mbili ambapo timu za Everton, Man City na Sunderland pamoja na wadau wengine walijitolea kumchangia lakini baadae jopo la madaktari lilitoa taarifa ya kushindikana kwa matibabu hayo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.