Nay wa Mitego "Siwezi Kushushwa na Mr T Touch Kwenye Muziki" - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nay wa Mitego "Siwezi Kushushwa na Mr T Touch Kwenye Muziki"

Msanii wa muziki wa Hip Hop Emmanuel Elibariki a.k.a ‘Nay wa Mitego’ amesema hawezi kushuka kimuziki kwa kuachana na producer Mr. T Touchez na kusema kuwa hajawahi kuanguka katika muziki wake kutokana na maneno ya watu wanaomuombea mabaya.

Mr Nay amefunguka hayo wakati akijibu maswali ya wadau mbalimbali kwenye kipindi cha Kikaangoni kinachoruka mubashara kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV ambapo baadhi ya maswali yalihoji kuwa kuachana na aliyekuwa producer wake Mr. T Touchez ni kweli yamemshusha kimuziki?nae alijibu kwa kusema

“Siwezi kushuka kwa ajili ya maneno ya watu na mimi na kwa sababu mimi ninamuamini Mungu wa dunia yangu ambaye kila nikimuomba ananijibu kwa wakati. Pia mimi siyo msanii aliyedumaa hivyo hakuna mtu ambaye ana uwezo wa kubadilisha upepo wa muziki wangu. Si mnaona sijiwezi inakamata Top 10 vituo mbalimbali hivyo sijashuka kimuziki”. Alisema Nay wa Mitego.

Nay wa Mitego kwa sasa ngoma yake ya ‘Sijiwezi’ inafanya vizuri kwenye media zote hapa Bongo ukiachana na tu na wimbo huo kupokelewa vizuri na mashabiki wake lakini pia amepata Pongezi kutoka BASATA kwa kufanya kazi nzuri ya video ya wimbo huo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.