Nay wa Mitego Kuja na Kanisa Lake, ‘ Sio la Biashara Ila la Kumuabudu Mungu Aliye Hai ’ - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nay wa Mitego Kuja na Kanisa Lake, ‘ Sio la Biashara Ila la Kumuabudu Mungu Aliye Hai ’

Nay wa Mitego anasema anafungua kanisa lake la kumuabudu Mungu.
Amedai kuwa kanisa lake litakuwa si la biashara, bali la kumuadu mwenyezi Mungu aliye hai.
“Acha kanisa likamilike, mwenye Mungu asimamie tutajua nini kinaenda kutokea lakini sio kanisa kwaajili ya kupiga hela,” Nay aliiambia E-News.
Nay amedai kuwa mchungaji wa kanisa lake atakuwa tofauti na hatotegemea sadaka za waumini ili kuendesha maisha yake, bali kazi yake nyingine itakayoweza kumuingizia kipato.

Rapper huyo amejinadi kuwa anatarajia kupata waumini wengi kupitia kanisa lake na kwamba litakuwa chanzo cha mafanikio katika mambo yao.
Nay amedai kuwa kanisa lake litajengwa Mbezi ya Kimara jijini Dar es Salaam.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.