Nape Nnauye Ataka Zuio la TCRA la Kuzuia Online TV Lisitishwe. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nape Nnauye Ataka Zuio la TCRA la Kuzuia Online TV Lisitishwe.

Baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kutangaza zuio la uendeshaji wa runinga za mtandaoni (Online TV), Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametengua zuio hilo.

Mh.Nape amesema kuwa ameamua kusimamisha zuio hilo kwakuwa halitakuwa na tija kwa wakati huu kwani kanuni zinazotoa muongozo wa namna ya kuendesha maudhui ya mtandaoni bado ziko kwenye mchakato na hazijakamilika.

“Mpaka tutakapokamilisha kanuni ndipo tutakapokaa na wadau tuzungumze namna ya kuendesha hizo ‘online content’ zote. Serikali inafanya mchakato huo, tuko katika hatua za mwisho. Zitakapokamilika tutawaita wadau,” Nape Nnauye ameiambia Clouds FM.

Aliongeza kwa kusema “Hakuna sababu ya kuharakisha kwenda kuwafungia watu bila kuwa na sheria au kanuni ambazo zinalielezea jambo lenyewe,”.

Waziri huyo alifafanua kuwa ni lazima uendeshaji wa maudhui ya mitandaoni kwa wana habari ifuate kanuni na sheria na kwamba kanuni zinazokuja hazitakuwa na nia ya kuzuia bali kusimamia (regulate).

Alisema nia ya kuweka kanuni hizo ni kuhakikisha kunakuwa na uwajibikaji wa watumiaji wa maudhui ya mtandaoni na wanaoweka maudhui hayo na kwamba utaratibu huu hufanyika kote duniani.

Hivi karibuni, TCRA walitoa barua iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo ikiwataka wamiliki wa Runinga za Mtandaoni ambazo ni Global TV Online, Michuzi TV na Ayo TV kuzifunga runinga zao mpaka pale ambapo mamalaka hiyo takapokuwa imekamilisha kanuni za usajili kwa runinga hizo kulingana na sheria za nchi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.