'Mimi Nina Uwezo Mkubwa wa Kuwapatanisha Diamond na Alikiba' - Dullysykes. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

'Mimi Nina Uwezo Mkubwa wa Kuwapatanisha Diamond na Alikiba' - Dullysykes.

Kwenye vijiwe au maeneo wanayokaa wadau wengi wa muziki stori za Diamond Platnumz na Alikiba mara nyingi huzungumzwa na wengi wao wanatamani kuona Alikiba na Diamond siku moja wakiwa kwenye wimbo mmoja au kushirikishwa na mtu ili tu kurudisha ukaribu wao uliowahi kuwepo hapo kabla.

Dullysykes ni mmoja kati ya malegend wa muziki wa Bongo fleva ambapo yeye kaliona hili na amesema aliwahi kutaka kuwapatanisha kwenye wimbo wake wa Utamu ambao baadae aliwashirikisha Diamond na Ommy Dimpoz >> ’Nilitaka niwapatanishe kwenye Utamu lakini ikashindikana kwa upande wa Ali Kiba’

‘Upande wa Diamond yeye alikuwa amekubali kuingia studio na tukafanya. Ali Kiba yeye ndio ikashindikana,mimi nina uwezo mkubwa wa kuwapatanisha Ali Kiba na Diamond lakini siyo sasa hivi kwa muda huu siyo kwasababu nikianza kusema nawapatanisha hata biashara za pande zote mbili zitakuwa zimevunjika tena’

‘Kwa ugomvi uliofikia sasa ni ugomvi mkubwa sana ni vita siyo ugomvi tena kwa kuwa ni vita kupatanisha vita ni ngumu sana mimi sitoweza ila nitasubiri miaka kadhaa ipite ili niwapatanishe’

‘Alikiba nilikuwa namwambia kuhusu kolabo hiyo lakini ananirusha mara leo mara kesho mwisho wa siku akashindwa akaniambia kwamba sitaweza, alikuwa anajua kama nitamshirikisha Diamond pia lakini pia simlaumu haikuwa kwa ubaya kwasababu stage waliyokuwa wamefikia ni stage ya ugomvi’

‘Siwezi kusema nimlaumu Ali Kiba au nimlaumu Diamond kwanini amegombana na Ali Kiba au Ali Kiba kwanini amegombana na Diamond,ugomvi wa Diamond naAli Kiba ndio ulioleta chachu kubwa katika mziki wa Tanzania kukua si unaona jinsi huyu anafanya hivi huyu naye anafanya hivi kila mtu anapigana kwa upande wake’

‘Kwa upande wangu naona ndo imekuwa kitu kizuri vijana wengi wanapigana nao hawataki kuwa kamaAli Kiba na Diamond so mziki unakua’ – Dullysykes.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.