‘Marry You’ ya Diamond na Ne-Yo Kuanza Kuoneshwa Leo Kwenye Trace TV. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

‘Marry You’ ya Diamond na Ne-Yo Kuanza Kuoneshwa Leo Kwenye Trace TV.

Baada ya takriban miaka miwili tangu urekodiwe, hatimaye wimbo wa Diamond aliomshirikisha msanii wa Marekani, Ne-Yo, ‘Marry You’ unatoka rasmi, Jumatano hii.

Ni Trace TV ndiyo inakuwa ya kwanza kuionesha video hiyo. Kituo hicho cha runinga kimepost video ya staa huyo kwenye Twitter akielezea kuhusu kurushwa kwa video yake.

Tayari Youtube wimbo huu umewekwa kwenye utitiri wa channel lakini ulikuwa haujawahi kuachiwa rasmi. Video ya wimbo huo ilifanyika Marekani mwaka jana.

Awali, video ilikuwa itoke mapema zaidi, lakini ratiba ilibadilika baada ya ziara ya Ne-Yo Uingereza ambayo amemuongeza Diamond kusogezwa mbele. Kwa sasa ziara hiyo itaanza Machi 29 na kufikia mwisho April 8 ya mwakani.

Awali ziara hiyo ilitarajiwa kuanza Jumatano ya Disemba 7 kwenye ukumbi wa Clasgow Barrowland na kufikia mwisho Disemba 14 ya mwaka jana.

Kupitia mtandao wa Instagram, Ne-Yo aliandika, “The December dates have been postponed! But don’t worry U.K. I’m still headed your way with NEW DATES and my bro @diamondplatnumz. 2017, let’s turn up! Tickets available at RoboMagicLive.com #NEYOUKLive.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.