Madee Ashambuliwa Insta Kisa 'Chura' ya Snura - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Madee Ashambuliwa Insta Kisa 'Chura' ya Snura

Msanii wa muziki Madee Ally ameshambuliwa na mashabiki kupitia mitandao ya kijamii baada ya kuonyesha hakupendezwa na kitendo cha Snura kushangilia wimbo wake ‘Chura’ kuimbwa na mtayarishaji wa muziki na msanii wa Nigeria Jon Jazzy kupitia mtandao wa Instagram.

CEO huyo wa Mavin Records alipost kipande hicho cha video Instagram akiimba wimbo huyo wa Snura kitendo ambacho kiliwavutia mashabiki wengi wa muiambiji huyo.

Hata hivyo mmoja kati ya wasanii wa Tanzania, Madee ameonyesha hakupendezwa na kitendo cha muimbaji huyo wa Chura kushangilia hatua hiyo huku akidai kuna wasanii wengi wa TZ wanaimba nyimbo za wasanii wa nje lakini wao hawaonyeshi kushangilia.
“Hivi ni ajabu sana Don jaz kuimba nyimbo ya snura eeh..mbona km bado tunajichukulia poa!!!mara ngap tunaimba na kucheza nyimbo zao!!,” alitweet Madee.
Baada ya kauli hiyo Snura alirudi na kuijibu tweet hiyo kwa kudai muimbaji huyo wa wimbo, Hela hajui uzito wa jambo alilolifanya Don Jazzy.
“Mpaka ukiona watu tunashungulika nae ujue kuna kitu ambacho macho yako yamefeli kuona.. haijalishi nass tunaimbaga au tunacheza za kwao, jamani chura huyo mama chura huyo @madeeali,” alijibu Snura kupitia Instagrama.
Kauli ya Madee iliendelea kutengeza malumbano kupitia mitandao ya kijamii, huku mashabiki wengi wakiipinga kauli ya Madee. Angalia baadhi ya maoni hayo.
carrymastory
@madeeali Acha roho mbaya wewe hakuna hata msanii wa bongo hapa hapa aliwahi kuposti anaimba nyimbo yako Itakuwa kenya au Nigeria Mxeeew kama huna chakuongea siukae tu Kimya Roho mbaya ya nini wakati hakuna dalili yoyote ya nyimbo yako kufika Naija.

gotfrid_brighton

Tatizo la @madeeali uwaga anakurupuka akitoka kuvuta bangi ndio anacomment.
nanajmatimati
Mie nimependa jamani hebu jiulize nyimbo ngapi za tz anazijua kuziona na kuzisikiliza ! Tena yuko happy inaonesha kuna kitu amekaa kakitafakar sio bure ! Hebu ashum wewe kama wee wimbo huna apteiti nao unaanzaje kuchukua simu nakufanya kama donjaz  @snuramushi hiyo ni hatua mama Tena kubwa usishangae hata beyonce nae akafanya hivyo ! Yule ni producer tena mkubwa !’ Kwa sasa tambua yule ni fans wako !eeeee churaa ananesanesa churaaa kanichekesha alivyoanza kuyarudi

clarahoka

Madee hajashangaa wimbo wa Snura kuimbwa na Don Jaz jamani, embu someni vizuri post yake… Yy mwenyewe kakubali maana ata ss tunaimbaga nyimbo zao so wao kuimba zetu sio big issue

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.