Machache ya Kuyajua Kumhusu Bob Marley. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Machache ya Kuyajua Kumhusu Bob Marley.

Kama hayati Bob Marley angekua hai leo hii angekua anaadhimisha miaka 72 ya uwepo wake duniani lakini katika maisha yake aliyowahi kuishi kuna vitu inabidi uvifahamu kutoka kwake inawezekana unasikiliza muziki wake na kuukubali lakini huvifahamu.

Miongoni mwa vitu muhimu vya kufahamu ni kuwa Bob Marley alizaliwa Jamaica na ilikua Feb 06 1945 na kufariki May 11 1981,baba yake Bob Marley alikua mzungu,ingawa wakati wa uhai wake hakupenda kufahamika kama mzungu alipenda kutambulika kama Muafrika mweusi (Black African).

Bob Marley mpaka Mungu anafariki idadi sahihi ya watoto wake haijatoka au kutangazwa ingawa watoto wanaotambulika mpaka sasa ni 11 tu ambao ni Sharon,Cedella,David ‘Ziggy’,Stephen,Robert ‘Robbie’,Rohan,Karen,Stephanie,Julian,Ky-Mami na Damian.

Mnamo mwaka 1979 ikiwa ni siku moja kabla ya Tamasha la Smile Jamaica, Bob Marley alivamiwa na kupigwa risasi mkononi ingaw alifanikiwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo,maneno ya mwisho ya Bob Marley kwa mtoto wake Ziggy kabla hajafariki yalikuwa ‘Money can’t buy life’.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.