Maamuzi Yaliyofanywa na Chris Brown Kuhusu Karrueche. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Maamuzi Yaliyofanywa na Chris Brown Kuhusu Karrueche.

Taarifa iliyotoka hivi karibuni inasema kuwa Mkali Chris Brown ameamuriwa kukaa mbali na aliyewahi kuwa mchumba wake Karrueche Tran, baada ya karrueche kumshtaki kisheria akisema Chris brown aliapa kumuua na alishawahi kupigwa kipindi cha nyuma.

Madai hayo ya Karrueche baada ya kuapishwa na hakimu mapema mwezi huu alinukulia akisema ‘Chris aliwaambia watu wachache kwamba alikuwa anataka kuniua’ kisha akasema Chris aliwaambia marafiki zake kuwa kama hawezi kuwa na Karrueche basi hakuna mwingine ambaye angemuweza.

Baada ya post hiyo Chris Brown alicomment kwenye post hiyo.

Vitisho vingine ambavyo aliwahi kupewa ni kutishiwa kuuwawa kwa kupigwa risasi,ingawa miaka michache iliyopita Karrueche anasema aliwahi kupigwa mara mbili na kusukumwa kwenye ngazi,hii ilikua muda mfupi baada ya Chris kuachiwa na Polisi kwa kosa la kumpiga Rihanna.

Nyaraka za kisheria pia zinadai Chris ametishia kudhuru marafiki zake Karrrueche na hata hivi karibuni alishawahi kumtupia kinywaji mmoja ya marafiki zake,Karrueche bado ana wasiwasi kuwa sasa Chris brown anayachukulia hatua maneno yake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.