List ya Wasanii Waliopo Chini ya So Famous Entertainment, Label ya Jay Moe - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

List ya Wasanii Waliopo Chini ya So Famous Entertainment, Label ya Jay Moe

Rapper Jay Moe amekuwa ni moja kati ya wasanii wachache wa zamani ambao mpaka sasa wanafanya vizuri. Hii ameionesha kwenye ngoma yake ya Pesa ya Madafu na ngoma alizoshirikishwa kama Mwendo Tu n.k.

Licha ya hivyo Jay Moe ameweka wazi kile ambacho amekuwa akikiongelea mara nyingi sana, So Famous Entertainment. Moe amesema, SFE ni management company ambayo itawasaidia wasanii wengine.

“Hiyo ni label ambayo itasaidia wasani wengi tu kama akina Deddy, kina Climax Bibo, kina Mansu Li na wengine,” amesema.

“Kwahiyo mwendelezo utakuwa mzuri kwasababu mimi mwenyewe siwezi kufanya milele ntahitaji na mimi nisaidie kama nilivyosaidiwa na P-Funk na vitu kama hivyo kuweza kupass kijiti kwa watu wengine. Lakini siwezi kukipass hicho kijiti kama upande wangu haujakaa kwasababu wao wanahitaji muongozo wangu, kwahiyo tutataka kutengeneza kwanza huo muongozo wangu uwe vizuri ili iwe rahisi kwao kuweza kuchomoka pia.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.