'Kama Utanipenda' ya Darassa Yaungana na Muziki na Too Much Kwenye Klabu ya Milion Viewers Youtube - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

'Kama Utanipenda' ya Darassa Yaungana na Muziki na Too Much Kwenye Klabu ya Milion Viewers Youtube

Darassa anazidi kujitengenezea rekodi katika muziki wake. Video ya wimbo wake ‘Kama Utanipenda’ aliomshirikisha Rich Mavoko umefikisha views milioni moja katika mtandao wa Youtube.

Video hiyo ilitoka Februari 12, mwaka jana imetazamwa mara 1,003,884 mpaka sasa kwenye mtandao huo. Hii ni video ya tatu ya rapper huyo kutazamwa zaidi katika mtandao wa Youtube baada ya ‘Muziki’ ambayo imetazamwa zaidi ya mara milioni nne na ‘Too Much’ iliyotazamwa iliyotazamwa mara 1.6 milioni.

Kwa taarifa yako tu, Darassa ndiye rapper pekee Tanzania mwenye rekodi hiyo.

Lakini hakuna ubishi ‘Muziki’ ndio wimbo ambao Darassa anatakiwa kuupa heshima kubwa kwa kuwa umempandisha juu zaidi na kuziinua nyimbo zake zilizopita kuanza kuonekana tena mpya.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.