Huu Ndiyo Ushauri wa Shamsa Ford kwa Wasanii Wakike Nchini. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Huu Ndiyo Ushauri wa Shamsa Ford kwa Wasanii Wakike Nchini.

Msanii wa Filamu nchini Mwanadada Shamsa Ford ametoa ushauri kuntu kwa wasanii wenzake wa kike hususani waigizaji wa Filamu wa kuwataka waolewe.

Shamsa Ford akizungumza kwenye kipindi cha Double XL cha Clouds FM amesema wanawake wengi walio kwenye Tasnia hiyo wanasubiri mpaka wapate mabwana wenye pesa ndiyo wakubali kuolewa,kumbe hawajui hata hizo mali walizonazo hawajazipata peke yao hivyo amewashauri kukubali kuolewa na mwanaume yeyote ambae atampenda kwa hali yoyote aliyonayo.

“Mimi nawashauri wasanii wenzangu wa kike wakimpata mtu mwenye mapenzi ya dhati ni bora kuolewa tuu,kwani kusubiri mpaka kumpata mwanaume tajiri aje akuambie anakupenda !! ndio ukubali bila kujua tayari kuna mtu katoka nae mbali mpaka kuwa tajiri kwahiyo nawashauri msichague chague wanaume itawa cost“ amesema Shamsa Ford.

Kwa sasa Shamsa Ford anatumikia ndoa na mfanyabiashara maarufu jijini Dar es salaam Chidi Mapenzi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.