Hizi Ndiyo Sababu za Wema Sepetu Kuhamia CHADEMA. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hizi Ndiyo Sababu za Wema Sepetu Kuhamia CHADEMA.

Miss Tanzania mwaka 2016 Wema Sepetu ambae wengi wanajua kuwa ni mkereketwa na Kada wa Chama cha Mapinduzi kwa sasa sio kada tena wa chama hicho bali ni Mwanachama rasmi wa Chama kikuu cha Upinzani nchini CHADEMA.
Wema Sepetu katikati akiongea na Waandishi wa Habari.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa ameambata na mama yake mzazi nyumbani kwao Sinza Jijini Dar es Salaam, Wema amesema sababu kubwa ya kuhamia CHADEMA ni ili kupata nafasi ya kupigania demokrasia anayodai kuwa inapotea nchini Tanzania Tanzania.

Sababu nyingine aliyoieleza Wema ni kutelekezwa na CCM licha ya kujitolea kutoa mchango wake kwa chama hicho wakati wa kampeni cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kiasi cha kuwa hatarini kumwagiwa tindikali visiwani Zanzibar.

“Kuanzia sasa mimi siyo tena mwanachama wa CCM, na muda mfupi ujao nitachukua kadi yangu ya CHADEMA… Nimeamua kuingia CHADEMA kwa sababu nataka kupigania demokrasia, laiti ningejua, ningeingia zamani sana, najua nimewahi kusema kuwa nitakufa nikiwa CCM, lakini sikujua kama itakuwa hivi, laiti ningejua mapema basi nisingesema vile na ningejiunga CHADEMA muda mrefu sana“. Amesema Wema Sepetu

Amesisitiza kuwa hajaamia CHADEMA kwa sababu ya pesa kama ambavo imekuwa ikidaiwa, bali ni kwa ajili ya kupigania demokrasia, na kuweka wazi kuwa kuanzia sasa ameingia kwenye mapambano ya kupigania demokrasia akiwa kwenye chama ambacho anaamini kuwa ni chama peke chenye uwezo wa kurejesha demokrasia inayopotea.

“Sijachukua pesa yoyote kutoka CHADEMA, kama nimechukua hata shilingi 10,000 ya CHADEMA basi kaburi la baba yangu huko Zanzibar litikisike” – Amesema Wema

Wema pia amejibu kuhusu baadhi ya wasanii kuidai CCM na kumesema “Ni kweli kuna madeni mengi wasanii tunaidai CCM, lakini kila wakati tukidai tunaambiwa tukamdai JK”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.