Gigy Money Afunguka Kisa cha Kugombana na Mpenzi Wake Mo J. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Gigy Money Afunguka Kisa cha Kugombana na Mpenzi Wake Mo J.


Mtangazaji wa kipindi cha Lavidavi cha Choice Fm, Gigy Money amefunguka kwa kueleza kilichosababisha yeye na aliyekuwa mpenzi wake Mo J wakagombana na kuachana licha ya kuwa alivalishwa pete ya uchumba siku za hivi karibuni.

Akifanya mahojiano wiki hii, Gigy amedai aliumizwa na kitendo cha kupigwa na mpenzi wake huyo baada ya kugundua amechepuka.

“Kuna mambo yalitokea, Mo J alichepuka mimi nikamshtukia, kwa baada ya kumwambia akaanza kunigiga,” alisema Gigy Money.

Aidha, Gigy Money alisema kuwa anamshukuru Mungu kuwa sasa yeye na mpenzi wake huyo wapo sawa.

“Lakini namshukuru mungu yameisha baada ya mimi pia kuchepuka, kwa sababu labda alikuwa hajui maumivu ya kuchepuka, kwahiyo sasa hivi tupo sawa” alisema Gidy.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.