Gerard Pique Arejesha Matumaini Barcelona - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Gerard Pique Arejesha Matumaini Barcelona

Gerard Pique

Klabu ya Barcelona kwa sasa ina matumaini tele kufuatia beki wake mahiri Gerard Pique kuanza mazoezi wakati wakielekea katika mchezo wao wa kesho wa nusu fainali ya mkondo wa pili ya Kombe la Mfalme dhidi ya Athletico Madrid.

Beki huyo alilazimika kutolewa wakati wa mapumziko katika ushindi wa mabao 3-0 waliopata Barcelona dhidi ya Athletic Bilbao Jumamosi iliyopita baada ya kupata majeruhi ya msuli.

Meneja wa klabu hiyo Luis Enrique amesema majeruhi hayo ya Pique yalichangiwa kwa kiasi kikubwa na ratiba ngumu waliyonayo.

Hata hivyo, nyota huyo wa kimataifa wa Hispania alifanya mazoezi na wenzake mapema leo na kuna kila dalili atakuwepo katika mchezo huo wa kesho ambao Barcelona wanaongoza kwa mabao 2-1 waliopata katika mchezo wa mkondo wa kwanza.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.