Fid Q Amjibu Young Killer Baada ya Kuambiwa Hajui Ku-freestyle. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Fid Q Amjibu Young Killer Baada ya Kuambiwa Hajui Ku-freestyle.

Kwenye stori zilizotoka na kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ni pamoja na hii ya Young Killer kusema kuwa hajawahi kumkubali Rapa Fid Q kwenye uchanaji wa mitindo huru ‘freestyle’

Kwenye nukuu yake amesema aliyotoa akiwa East Africa Radio Young Killer alisema >> ’Sijawahi kumkubali Fid Q kwa ‘free style’ sababu sijawahi kumuona akifanya hivyo ila niliowahi kuwaona wakifanya mitindo huru nampenda sana Nikki Mbishi, GodZillah pamoja marehemu Albert Mangwea’

Baada ya maneno hayo DizzimOnline imemtafuta Fid Q mwenyewe na kakubali kuelezea >> ’Itabidi weekend moja nikiwa sina shughuli ya kufanya nimuite hapa nyumbani halafu nimpigie freestyle kama Buku hivi huku nikiwa nimemuwashia kamera na kuweka tukio live on instagram’.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.