Feza Kessy 'Napenda Mwanaume Ambaye Havai Skini Jinzi na Ambaye Sio Chips Mayai' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Feza Kessy 'Napenda Mwanaume Ambaye Havai Skini Jinzi na Ambaye Sio Chips Mayai'

HII ikufikie wewe mpenda burudani na ubuyu wa town! Msanii wa Bongo Fleva, Feza Kessy amepigwa kibuti siku kumi kabla ya kufi kia Sikukuu ya Wapendanao ‘Valentine’s Day’.

Akizungumza na E’bana Dah hivi karibuni ndani ya Ukumbi wa Club Next Door uliopo Masaki jijini Dar, Feza ambaye pia alikuwa mshiriki wa Shindano la Big Brother Africa 2013 ‘The Chase’ alisema, kwa sasa ameamua kupumzika kidogo mpaka moyo utulie.

“Tangu niachwe kabla ya valentine nipo singo sasa hivi kimya kimya na bado nina maumivu labda hapo baadaye,” alisema Feza. 


Alipobanwa ni mwanaume wa aina gani anampenda alisema:

“Napenda mwanaume ambaye havai skini jinzi, nataka mwanaume apige timba (viatu aina ya mabuti) na tisheti. Siyo mwanaume anakula chipsi mayai. Sitaki awe milionea, pesa kidogo ya kutumia inatosha, kikubwa aniheshimu na asiwe mshamba wa mademu wa kutaka achepuke wakati yupo na mimi.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.