Diamond Platnumz Aripoti Kituo Cha Polisi, Atoa Onyo - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond Platnumz Aripoti Kituo Cha Polisi, Atoa Onyo

Diamond amefunguka na kueleza nini kilitokea baada ya jioni ya leo kusambaa picha zinazomwonyesha akihojiwa na jeshi la polisi.
Diamond akitoa maelezo mbele ya askari.

Muimbaji huyo amedai alienda polisi kujieleza kwa jeshi la usalama barabarani baada ya jeshi hilo kudaka clip yake ya video inayomwonyesha aliendesha gari huku akiwa hajavaa mkanda.

Diamond ametoa taarifa hii;

Leo nilireport kituo kikuu cha polisi wa usalama barabarani kutokana na Vidoe Clip tuliyopost naendesha gari barabarani bila kufunga mkanda na pia kuachia usukani na kucheza…. Nikapewa Onyo na Kulipa faini kulingana ya Mujibu wa sheria… tafadhali watanzania na Vijana wenzangu… tuhakikishe tunafunga mikanda pindi tupandapo na tuendeshapo Magari Maana ni Hatari kwa Maisha yetu na inaweza kukupeleka kunyea debe pia.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.