Dada Yake Diamond Azuiwa Kumuona Zari, Kisa Hiki Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Dada Yake Diamond Azuiwa Kumuona Zari, Kisa Hiki Hapa

Ukistaajabu ya Musa Utaona ya Firauni, hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mzazi mwenza wa mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘The Boss Lady’ kuwa na masharti magumu ya kumfikia pale uwapo na hitaji la kuonana naye baada ya kutua nyumbani kwa Diamond, Madale jijini Dar.

Hivi karibuni dada wa aliyejitambulisha kuwa ni wifi wa Zari alijikuta kwenye simanzi baada ya kupewa masharti ya aina yake na mlinzi wa getini nyumbani kwa Diamond alipokuwa amekwenda kumtembelea.

Aliambiwa ili aweze kumuona Zari, anatakiwa kuwa na barua kutoka serikali ya mtaa ili kumtambulisha kabla ya kupata ruhusa ya kuonana na mama huyo raia wa Uganda au uwe umewasiliana na Diamond mwenyewe na akakiri kukutambua.

Kamera za makachero wa Oparesheni Fichua Maovu ya Global Publishers (OFM) zilifanikiwa kulinasa tukio zima baada ya wifi huyo aliyedai ametokea Tandale nyumbani alipokulia Diamond, kuwaomba OFM wampe kampani alipokuwa anaenda Madale. “Nimeambiwa nyinyi OFM mnapajua vizuri kwa Diamond sasa naomba mnipeleke nikamuone wifi yangu maana nimejaribu kutafuta mawasiliano ya Diamond bila mafanikio.

Unajua Diamond tumekua naye Tandale sasa japo si ndugu yangu wa damu  lakini Zari ndiye wifi yetu kutokana na ukaribu tuliokuwa nao,” alisema wifi huyo.

OFM iliongozana na dada huyo hadi nyumbani kwa Diamond lakini bahati haikuwa yake maana alikutana na vizingiti vya hali ya juu getini:

Wifi: Habari zako.

Mlinzi: Poa nikusaidie nini?

Wifi: Naitwa (anataja jina lake) naishi Tandale ni dada yake na  Diamond wa hiyari, nimekuja kumsalimia wifi yangu Zari.

Mlinzi: Iko wapi barua ya serikali ya mtaa?

Wifi: Kwani kuja kumsalimia wifi yangu hadi niwe na barua kutoka serikali ya mtaa ndiyo utaratibu gani huo?

Mlinzi: Huo ndiyo utaratibu na ni vizuri ukatambua utaratibu uliowekwa na wahusika wa mji huu, bila barua kutoka serikali ya mtaa unakotokea huwezi kuingia ndani na siyo wewe tu huu ni utaratibu ni wa kila mtu.

Hadi OFM wanaondoka nyumbani hapo, wifi huyo alishindwa kuingia baada ya kusema hawezi kwenda serikali ya mtaa kwa ajili ya jambo hilo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.