Chelsea Kileleni Mwa Ligi kwa Pointi Tisa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Chelsea Kileleni Mwa Ligi kwa Pointi Tisa

Kipa wa liverpool Mignolet apangua mkwaju wa penalti uliopigwa na Diego Costa

Chelsea ililazimika kutoka sare dhidi ya timu ya Liverpool ilioimarika katika uwanja wa Anfield baada ya penalti ya Diego Costa kupanguliwa na kipa Simon Mignolet lakini bado wakaongeza uongozi wao katika kilele cha ligi ya Uingereza na pointi tisa.

Kipa wa Liverpool Mignolet alirekebisha makosa yake baada ya kupatikana amezubaa na mkwaju wa adhabu wa David Luiz.

Kichwa cha karibu cha Georginio Wijnaldum kunako dakika ya 11 baada ya muda wa mapumziko kiliipatia Liverpool sare waliohitaji, na hivyobasi kusitisha msururu wa matokeo mabaya ambao ulikuwa umekumba timu hiyo.

Matokeo hayo yalisababisha kubanduliwa kwa timu hiyo katika kombe la EFL pamoja na lile la FA.

Hatahivyo ingekuwa bora zaidi kwa Chelsea na vibaya zaidi kwa Liverpool baada ya Costa kuangushwa na Joel Matip dakika 14 kabla ya kukamilika kwa mtanange huo.

Refa Mark Clattenburg alitoa penalti kwa upande wa Chelsea lakini kipa Mignolet akaokoa penalti hiyo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.