Ben Pol Asema Wimbo Wake Phone Unafanya Mahusiano Mengi Yadumu. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ben Pol Asema Wimbo Wake Phone Unafanya Mahusiano Mengi Yadumu.

Huu ni msimu wa Valentine’s, msimu wa wapendanao. Nyimbo nzuri za mapenzi, ni moja ya vitu vinavyonogesha mahusiano hususan msimu huu wa Valentine’s, lakini swali la wapenzi wa muziki mzuri limekuwa ni Je,ngoma ya Phone ya Ben Pol inafaa kutumika msimu huu?

Ben Pol yeye binafsi anategemea ngoma hiyo kutumika Valentine’s Day.

“Phone inasaidia mapenzi yadumu. Kwasababu kama haumchunguzi sana mpenzi wako ina maana maisha yenu yatakua na furaha,amani nini hamna migogoro. Kwahiyo Phone pia inahusika,” amesema Ben Pol.

Video ya ngoma hiyo inafanya vizuri kwa sasa na mpaka sasa imefikisha zaidi ya views 69,000 huko Youtube tangu itoke mwezi uliopita.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.