Barakah The Prince 'Mwezi Ujao Lord Eyes Anaachia Wimbo' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Barakah The Prince 'Mwezi Ujao Lord Eyes Anaachia Wimbo'

Hii inawezekana ikawa kama ni majibu ya kile kilichozungumzwa na Nay wa Mitego jana Jan 07 kumhusu Barakah The Prince kumsaini Lord Eyes na Nay wa Mitego alisema kitendo hicho ni sawa Kipofu na Kiziwi.

Barakah The Prince kupitia XXL ya Clouds FM amesema >> ’Siwezi kuongelea mambo ya watu ambao sina faida nao,mimi nina plan zangu na Lord vitu vikiwa tayari nitazungumzia, siwezi kumuongelea mtu ambaye simfahamu’

‘Mwezi ujao Lord anaachia wimbo wake,video kila kitu viko tayari kwa hiyo tunasubiri kuna vitu fulani tunavimalizia,nakaa na Management yangu kwa sababu mimi sio nitakayekua namsimamia Lord kutakua kuna watu kwa hiyo naviweka sawa vya usimamizi wa kazi zake’

‘Wimbo wake soon utatoka na mwezi wa tatu hauiishi’ – Barakah The Prince.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.