Amber Lulu Adai Anapenda Kufanya Muziki Kuliko Kuwa Video Queen - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Amber Lulu Adai Anapenda Kufanya Muziki Kuliko Kuwa Video Queen

Video Vixen aliyejizolea umaarufu mkubwa hapa Bongo, Amber Lulu mwaka jana mwishoni alifungua page mpya ya vipaji vyake kwa kuachia ngoma yake ya kwanza tangu tuanze kumfahamu.

Ngoma hiyo iliwashtua watu wengi,lakini good news ni kuwa comments nyingi zilimtaka aingie rasmi kwenye muziki na kuachana na mishe nyingine kama u-video Queen.

Kwenye Interview na Dizzim Online,Amber Lulu ameweka wazi kuwa anapenda zaidi kufanya muziki kuliko upande aliokuwepo mara ya kwanza.

“Mimi binafsi nimepanga niingie kwenye muziki. Ni kitu ambacho nakifanya kila siku,yaani muziki sasa hivi ni kama maisha yangu ya kila siku..nakomaa mwanzo mwisho,” amesema Amber.

Mrembo huyo amedai kuwa tayari ana ngoma nyingine ambayo ataiachia muda wowote.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.