Alikiba Kutua Dar Jumanne Hii, Kula Dinner na Wadau muhimu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Alikiba Kutua Dar Jumanne Hii, Kula Dinner na Wadau muhimu

Baada ya kufanya ziara yenye mafanikio nchini Afrika Kusini, Alikiba anatarajiwa kutua Dar es Salaam, Jumanne hii.

Kiba na timu yake watatua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, saa nane mchana ambapo anatarajiwa kupata mapokezi makubwa.

Baada ya mapokezi hayo, Kiba atakula chakula cha usiku na wadau muhimu wakiwemo wanahabari kwenye hoteli ya Double Tree. Jumatano asubuhi atapaa tena hewani kuelekea Marekani kwa ziara yake ya huko kwenye majiji kadhaa.

Pamoja na ziara yake hiyo nchini Afrika Kusini, Alikiba alikabidhiwa tuzo yake ya MTV EMA pamoja na kupewa tuzo na label yake ya Sony Music baada ya wimbo wake Aje kufikisha views milioni 5 kwenye Youtube.

Pia alifanikiwa kumalizia kurekodi collabo yake na mwanamuziki mkongwe, Yvonne Chakachaka.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.